Ibada Ya Kiswahili
Jumapili | 10am | Living Room 

 

Utaratibu wa kuandikiza watoto kwa kompyuta:

1. Kanisa ya Bethesda imeweka kompyuta tano za kuandikiza watoto siku za kanisa Jumatano (Wednesday) na Jumapili (Sunday).

2. Wageni watapata usaidizi kwa kompyuta mbili zilizo na wafanyi kazi, hawa wafanyi kazi watasaidia wageni kuandikiza watoto.  Zile kompyuta  zingine tatu hazina wafanyi kazi lakini wale wenye si wageni wanaweza kuzitumia.

3. Mzazi ama yule anayeleta mtoto kanisani atapewa karatasi ambayo iko na sehemu ambazo nilazima zijazwe ndio jina la mtoto liwekwe kwa kompyuta. Watoto wenye umri  chini ya miaka kumi na sita wa familia moja wanaweka kwa karatasi moja.

4. Kwa ajili hii, inabidi yule anayeleta mtoto awe na majina ya mtoto, tarehe ya kuzaliwa ya mtoto, darasa la mtoto, anwani penye mtoto anaishi na nambari ya simu ya mzazi.

5. Mzazi akimaliza kuandika hayo yote kwa karatasi, mfanyi kazi ataingiza majina kwa kompyuta na beji mbili zitatokezea kwa printer. Beji ya kwanza itaweka kwa shati ya mtoto, beji ya pili itapewa mzazi ama yule atakaye kuja kumchukua mtoto baada ya ibada.

6. Inabidi mazazi ama yule ambaye atakuja kumchkua mtoto aweke beji la pili vyema, ndio ibada ikimalizika aweze kupeana hili beji kwa darasa la mtoto ndipo aweze akumchkua mtoto.

7. Baada ya wiki tatu kuandikiza watoto, majina ya watoto yatapatikana kwa kompyuta. Baada ya hizi wiki tatu, Mzazi anaweza pata beji bila usaidizi wa mfanyikazi.

8. Kile mzazi atafanya ni kuingisha alfabeti chache za jina la mwisho la mtoto katika kompyuta, kwa mfano tuseme jina la mtoto ni 'Hana Kadeba' Mzazi ataingisha 'KADE ama "KAD" kwa kompyuta na vile vile ataona majina ya Hana Kadeba. Mzazi ataweka alama ✅ kwa jina na aendlee kuchagua 'GO' kwa kompyuta hadi beji mbili zitokezee kwa printer.

9. Vile vile beji ya kwanza itawekwa kwa shati ya mtoto, na beji ya pili itabaki na yule ambaye atakuja kumchukua mtoto baada ya ibada.

10. Mtoto ataregeshwa kwa yule pekee anaye na beji ya pili.